SIN 14

SIN 14

Author:
Price:

Read more

SIN 14
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
Website……………………………………………… www.storyzaeddytz.com
ILIPOISHIA
Kelele za furaha zinazo sikika sebleni zikamfaya mrs Sanga kukurupuka ndani kwake na kukimbilia sebeeni. Mapigo ya moyo yakamstuka mara baada ya kukutanisha macho yake uso kwa uso na mume wake ambaye hajaonyesha sura yoyote ya kumchangamkia. RCP akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa pingu huku akimtazama mrs Sanga anaye shuka kwenye ngazi huku akilazimisha tabasamu la kinafki kwani shida zote zilizo tokea katika siku mbili hizi yeye ndio chanzo.
ENDELEA
“Ohooo pole sana mume wangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akimkumbatia mume wake. Nabii Sanga hakuonyesha kitu chochote kibaya kwa mke wake.
“Nashukuru mke wangu. Pole sana kwa kukuweka katika kipindi kigumu sana wewe na watoto”
Maneno hayo ya nabii Sanga yakamfanya RPC kurudisha pingu zake mfukoni huku akiwatazama.
“Pole sana na wewe mume wangu. Vipi hawajakuumiza?”
Mrs Sanga alizungumza kwa mahaba mazito ambayo kwa namna moja ama nyingine ni uigizaji.
“Nipo salama kabi.”
“Mzee nina weza kupata muda wa kuzungumza na wewe kwa dakika chache?”
RPC alizungumza na kumfanya nabii Sanga kumuachia mke wake. Wakatoka nje na kuingia kwenye gari la RPC.
“Ahaa natambua kwamba hili jambo nitakalo kwenda kukueleza kidogo linaweza kukustua mzee wangu. Ila sina namna zaidi ya kukuambia, ili kama nitaamua kwenda mbele zaidi ya hapa basi uwe umesha jiandaa kisaikolojia.”
“Niambie tu usiwe na hofu”
“Ili kukupata wewe, tulifanikiwa kumkamata kijana mmoja anaitwa Tomas, ni dalali na pia niligundua ni kijana wako wa karibu sana?”
“Yaa Tomas ni kijana wangu nina muamini sana. Kwa nini mume mkamata?”
Nabii Sanga aliuliza kana kwamba hajui ni kitu gani kinacho endelea.
“Ahaa…ngoja kwanza”
RPC alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni. Akaweka sauti ya mahojiano yake na Tomas. Nabii Sanga akajifanya akistushwa sana na kukiri kwa Tomas, ila ukweli ni kwamba ana fahamu kila kitu kinacho endelea kati ya Tomas na mke wake.
“Ohoo Mungu wangu nimpe nini huyu mwanamke?”
“Ndio hivyo, sasa yule kijana yupo mahabusu. Ila mke wako yupo uraiani, endapo tukimpeleka mahakamani kijana huyo na aka zungumza jambo juu ya mke wako, basi tambua mke wako ata tiwa nguvuni na atastakiwa kutokana na makosa yake na pia atatumikia kifungo jela na akitumikia kifungo jela, huduma yako ina mambo mawili, ina weaza kuyumba au kutoweka kabisa. Kwani itakuwani kashfa kubwa sana kwako na familia yako kwa ujumla na unavyo tambua Watanzania kwakukuza mambo, basi utapotea kinamna hiyo.”
Nabii Sanga akaka kimya huku akitafakari juu ya adhabu gani ambayo ana weza kumpatia Tomas kwani kazi aliyo wapo Rama D na wezake hawato weza kuifanya kutokana na Tomas kukamatwa na polisi na hadi sasa nabii Sanga hatambui kwamba Rama D na ndugu zake wamesha uwawa na askari.
“Una weza kunisaidia kazi moja RPC?”
“Kazi gani?”
“Nahitaji kijana huyo afe kabla ya kupelekewa mahakamani, je itawezekana”
“Kuwezekana ina wezekana mzee. Ila sikuzote vitu kama hivi vina kwenda kwa pesa maalumu ambayo itatufanya kujilinda hata pale likitokea la kutokea, ikiwemo kusimamishwa kazi au kushushwa vyeo”
“Una hitaji kiasi gani?”
“Acha nikajitafakari kisha nitakuambia kabla ya saa mbili asubuhi”
“Sawa, ila hakikisha kwamba mke wangu haguswi kabisa na tuhuma hizi. Pia nitumie audio hiyo kwenye email yangu”
Nabii Sanga akamtajia RPC email yake na akatumiwa sauti hiyo.
“Nashukuru sana”
“Ila ushauri ni mmoja sasa kuwa makini sana na mke wako. Hakikisha kwamba mke wako una muweka mikononi mwako vizuri la sivyo ata kuja kukudhuru ukiwa humo ndani kwako. Kama alifanikiwa nje, basi ndani ni rahisi zaidi ya nje.”
“Nimekuelewa RPC”
“Nashukuru kwa kunielewa mzee”
Nabii Sanga na RPC wakashuka kwenye gari na kuingia ndani. RPC akamuaga mrs Sanga na wanaye, kisha akaondoka huku nyumbani hapo wakiwaacha askari wawili, watakao linda hadi asubuhi kisha kuanzia hapo nabii Sanga ata endelea na maisha yake na familia yake kama kawaida na swala la ulinzi litakuwa juu yake mwenyewe.
“Vipi mume wangu ume kula?”
“Ndio nipo vizuri. Naombeni niende kupumzika”
“Sawa baba”
Nabii Sanga akapandisha gorofani huku mke wake akimfwata kwa nyuma.
“Simu yako ina salio?”
“Ndio”
“Wasiliana na sekretari. Muambie kesho saa nne asubuhi nahitaji kuzungumza na waandishi wa habari. Nahitaji kuwafahamisha waumini wangu kote duniani kwamba nipo salama”
“Kwa nini usisubiri subiri siku ya kesho ipite, ili urudi katika hali yako ya kawaida”
“Hali ipi ya kawaida?”
“Uzoee mazingira ya nyumbani na ujipange tena upya kisaikolojia kisha ndio uzungumze na waandishi wa habari”
“Sikiliza mama Juliethi. Kuna watu wamefunga na wana sali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba nina kuwa salama. Watu hao kitu cha pekee cha kuwalipa na waamini kwamba Mungu amejibu maombi ya vile wanavyo viomba ni mimi kesho kusimama mbele ya waandishi wa habari na kuwaleza nini kilinikumba ni nani aliniteka huku huyo aliye niteka akisaidiana na nani kwenye kuniteka. Na aliye toa wazo la mimi kutekwa pia nita muanika hadharani ili dunia nzima ijue adui yangu ni nani hata siku ikitokea siku nime pata madhara basi adui yangu ana kuwa wakwanza kukamatwa”
Fumbo la nabii Sanga likamfanya mrs Sanga kustuka sana. Mwili ukaanza kumtemeka kwa maana yeye ndio mtu aliye toa wazo la mume wake kutekwa. Tomas yeye ndio aliye tekeleza wazo hilo.
“Mpigie una nitolea nini macho?”
Mrs Sanga akachukua simu yake na kupigia sekretari wa kanisa lao.
“Ehee zungumza naye”
Mrs Sanga alizungumza hukua akimkabidhi mume wake simu hiyo na akaiweka sikioni mwake.
“Baba mchungaji”
“Naam”
“Ohoo asante Mungu upo hai. Hapa mama alipo niambia kwamba niandae kikao kesho, nilikuwa na kigugumizi huku nikijiuliza naandaa kikao na waandishi wa habari je usipo tokea nini nitajibu nini. Ila nina furahi sana kusikia sauti yako baba”
“Usijali kijana wangu. Watesi wangu walijiinua ila Mungu ambaye hashindwi na jambo aliweza kusimama kwangu na kunipigania na kama sikufa katika kutekwa huku. Basi siku ni kifa nitakufa kwa amani tena baada ya kupitisha ule umri wa miaka themanini ambao Mungu aliupanga juu ya wana damu wake”
“Amen amen”
“Basi fanya hivyo na kesho tatu asubuhi njoo nyumbani kwangu”
“Sawa baba”
Nabii Sanga akakata simu na kumrudishia mke wake.
“Kuna wakati wa kuliaaaaa…..wakati wa kuombolezaaaaa, ila adui yako ni mtu wa karibu….”
Nabii Sanga aliimba wimbo huo huku akivua nguo zake na kuelekea bafuni huku akimuacha mrs Sanga akiwa katika wakati mgumu sana wa kujitafakari kama hicho anacho kizungumza mume wake kipo kweli kichwani mwake au ana hisi tu.
***
Magreth akaamka asubuhi na mapema. Akapanga nguo zake zote ambazo ana hisi zina umuhimu kuingia kwenye ulimwengu wa maisha yake mapya ya utajiri. Alipo hakikisha kwamba ame chukua vitu vyake muhimu, akwaamsha mama Boka na wezake. Wakingia chumbani kwake huku kila mmoja akiwa na shahuku ya kujua ame itiwa nini.
“Jamani mimi nina hama. Kuna kitanda godoro, jiko hii meza na sofa hapo, muna weza kugawan kwa kuchukua au mukaviuza vitu hivyo na mukapata pesa mutakayo gawana”
“Ehee shosti bora kuviuza, itakuwa ni jambo zuri”
Mama Boka aliwahi kuzungumza na kuwafanya wezake wamtazame.
“Basi ngoja nitoe wazo. Viuzeni, kisha pesa itakayo patikana nyinyi mugawane sawa kwa sawa. Asitokee hata mmoja kuwazidi wezake”
“Hapo Mage umesema. Ila shosti kweli una taka kutuambia kwamba leo hii una hama na kutuacha huku uswahilini?”
“Ndio mbona hamuamini?”
“Yaani nina ona kama ni ndoto vile”
“Kwa nini?”
“Yaani una tuacha hivi hivi, sisi tuna zidi kufubaa tu hapa na huyu bibi Ngedere”
“Wala musijali. Nikiweka mambo safi nita waalika muje kupaona kwangu. Tena niandikieni namba zenu”
Magreth alizungumza na kumpatia mama Boka simu yake. Wakaanza kuandika namba zao za simu.
“Yaani kweli Mage mambo yamekubadilikia. Sijawahi kukuona ukimiliki smart phone. Nilisha kizoea kile kisumu chako cha nokia ya tochi”
“Hahaa kiobama?”
“Ndio, mwenyewe kile hata ukikiacha huko uwani hakuna ambaye alikuwa ana shuhulika nacho kukaiba”
“Hahaa ndio hivyo Mungu ninaye muomba sio wa mchezo mchezo. Siku akiamua kukufungulia manoti ya pesa, hakuna ambaye ana weza kuyazuia”
“Ila rafiki yetu tuambie siri ya kufanikiwa”
“Kuokoka tu, ndio siri ya kufanikiwa. Sasa nyinyi kaeni hapa kwa huyu mama mukichambana na kuzungumza mambo mabaya mwishowe. Mutaishia hapa hapa”
“Jamani kweli anacho kizungumza Mage. Tuache kukaa vibarazani na kuwachamba watu”
Magreth akampigia Sheby na kumuomba afike nyumbani kwake. Hazikupita hata dakika tano Sheby akafika nyumbani hapo. Mama Boka, akamsaidia Magreth kubeba begi hilo la nguo huku moyoni mwake akiwa ametawaliwa na wivu mkubwa sana. Magreth akagonga kwa nguvu mlango wa bi Ngedere.
“Nani huyo mja lanaaaa?”
Bi Ngedere alizungumza kwa kufoka na kuwafanya Magreth na wezake kucheka kichini chini. Magreth akagonga kwa nguvu hadi bi Ngedere akafungua huku akiwa amevimba kwa hasira. Bi Ngedere akatoa msunyo mzito huku akimpandisha na kumshusha Magreth.
“Nini na wewe?”
“Chukua funguo za chumba chako. Funguo nyingine utaichukua kwa mama Bakari pale, kuna vitu ndani ya chumba wakitoa basi watakupatia”
“Kisa funguo ndio una nigongea kama nime vamiwa?”
“Aha…jamani mbona hivyo. Una chukua au huchukui? Nakuachia banda lako la kuku nakwenda kuishi wanapo ishi watu sio hapa kwenye banda lako hili”
Magreth alizungumza kwa kejeli huku akimtazama mwana mama huyo.
“Koma wewe nyumba yangu si banda la kuku?”
“Basi kama si la kuku, ni banda la njiwa. Hahaaa ulininyanyasa sana wewe mama, ukihisi kwamba sinto fanikiwa. Ila Mungu amenifanikisha. Pumbavu, sasa uwe na kinywa kizuri kwa hawa wapangaji wengine, siku ukiwakejeli haki ya Mungu, Tanroad watakuja kupitisha bararaba ya lami hapa mtaani na hili banda lako litavunjwa na hapo ndipo utakapo rudi kwenye maisha ya chini kabisa. Utajua shida ambazo tunapitia sisi wapangaji”
Magreth mara baada ya kuzungumza hivyo, akafungu pochi yake na kutoa noti tano za shilingi elfu kumi na kumpiga nazo bi Ngedere usoni.
“Tutaonana huko barabarani kwa maana sitaki siku nikiwa na gari langu nishindwe kukupa lifti”
Magreth akawafwata nje wapangaji wezake. Akaagana nao na kuingia kwenye gari.
“Sheby”
“Naam boss”
“Leo tuna mizunguko mingi. Nipeleke kwenye duka lenye hadhi ya kuuza furniture za ndani”
“Sawa hapa kwa haraka haraka ni Danube pale Mlimani City”
“Haya twende ila kabla ya hapo twende hospitali nikamuone mgonjwa wangu”
Magreth akafika hospitali ya Mwananyamala. Akaelekea kwenye chumba alicho lazwa Evans Shika. Wakasalimiana kwa furaha.
“Samahani juzi nilipata dharura na siku ya jana sikuweza kuonekana, kuna mambo kidogo yalitokea. Vipi una endeleaje?”
“Nina endelea vizuri sana. Dokta leo ameniambia kwamba wiki inayo fwata, nitapewa ruhusa”
“Habari nzuri sana Evans. Vipi wana kushuhulikia vizuri swala la chakula?”
“Yaa wameniletea chakula kizuri na nina kula kwa wakati kabisa”
“Nafurahi kusikia hivyo. Leo ratiba yangu ni ngumu kuna sehemu nina zunguka zunguka baadae nitapita kukuona”
“Sawa Mage. Leo ume pendeza sana”
“Kweli?”
“Ndio”
Magreth akajiona mwanamke mwenye bahati sana mara baada ya kusifiwa na Evans. Akatamani kumbusu ila akajikuta akishindwa kwani hakuna kitu chochote walicho weza kukubaliana kwenye mapenzi.
“Evans nina swali moja”
“Swali gani?”
“Una mchumba?”
“Hapana sina kwa kweli”
“SAWA”
Magreth alijibu huku akiwa na furaha sana. Akamuaga Evans na kurudi kwenye gari. Wakaelekea katika duka kubwa linalo uza vifaa vya ndani. Magreth aka nunu kila kitu anacho kihitaji katika duka hilo, kisha akapatiwa lori la usafiri la kubebea vitu hivyo kwani ni vingi sana. Akaongozana na watu wa lori hilo huku yeye na Sheby wakiwa mbele. Wakafika nyumbani kwake maeneo ya Kigamboni. Akawasimamia watu wa kampuni hiyo ya Danube, kumpangia kila kitu alicho kinunu dukani kwao. Ndani ya muda mfupi nyumba hiyo tayari ikawa imebadilika, huku kila mmoja akisifia kwamba imepangwa vizuri.
“Sheby hapa ni kwangu”
“Aisee ina maana huto uza tena maandazi?”
“Ndio, nitakuwa nina rudi kitaani kuwasalimia kama kawaida”
“Aisee kweli nina haki ya kukuita boss”
Kabla Mage hajazungumza kitu chochote simu yake ikaanza kuita. Akaitazama namba hiyo ngeni, akaipokea na kupewa maelekezo na mwanaume aliye jitambulisha kwa jina la Clayton ni ofisi zipi aende akachague gari, huku akidai ni agizo kutoka kwa nabii Sanga.
***
Mrs Sanga hadi kuna pambazuka hakuweza kupata usingizi kabisa. Mapigo yake ya moyo yamebadilisha muelekeo wake kabisa na amekuwa ni mtu aliye tawaliwa na mawazo kiasi kwamba ana tamani ardhi ipasuke ili immeze. Saa kumi na mbili asubuhi akaamka kitandani na kuelekea jikoni, akaandaa kifungua kinywa kizuri, kisha akarudi chumbani na kumuandalia mume wake suti anayo ipenda.
“Baba Julieth sasa hivi ni saa tatu kasoro amka ujiandae”
Nabii Sanga akamtazama mke wake kwa macho yaliyo jaa maswali. Akanyanyuka na kuingia bafuni, akaoga na kusafisha kinywa chake. Akafungua kabati la nguo na kutazama ni suti gani ambayo ata ivaa kwa siku hiyo.
“Baba Julieth nimesha kuandalia nguo hizo hapo”
Mrs Sanga alizugumza huku akujitahidi kutengeneza tabasamu la bandia. Nabii Sanga akazitazama nguo hizo alizo andaliwana mke wake, ila hakudhubutu kuzigusa. Akachukua suti nyingine na kutoka nazo hadi sebleni. Akambidhi mfanyakazi wake na kumuomba ampigie pasi. Akaingia jikoni, aka kaanga mayai mawili na soseji mbili.
“Dady leo ume amua kuingia jikoni?”
“Yaa mwanangu vipi chuo umekwenda siku mbili hizi?”
“Hapana sija enda. Askari walinizuia kwenda wakihofia usalama wangu”
“Ahaa..basi hakikisha leo una kwenda. Ulinzi wa malaika kutoka mbinguni utasimama juu yako”
“Sawa baba, ila mbona mama amesha andaa brakefast?”
“Ahaa nimependa leo nile chakula nitakacho pika kwa mkono wangu”
“Sawa dady I love you”
“I love you too daughter”
Julieth akambusu baba yake shavuni na kuelekea mezani. Mrs Sanga mambo yote yanayo endelea jikoni aliweza kuyashuhudia. Hali aliyo kuwa nayo mume wake hakika ikazidi kumuweka katika wakati mgumu sana. Wakati ambao hajui ni wapi ana anza kumuuliza mume wake, ikiwa ana tambua hali halisi iliyo mpata Tomas. Nabii Sanga akapata kifungua kinywa hicho. Akakabidhiwa suti yake na mfanyakazi wake na kuelekea chumbani, akavaa haraka haraka na kujiweka sawa.
“Baba Julitethi tuna weza kuzungumza”
“Kuhusiana na nini?”
“Mbona umerudi ila una onekana kuwa tofauti sana na awali?”
“Mkuu wa majambazi walio niteka aliniambia kwamba bosi wao ana hitaji nishikiliwe hadi wiki ijayo ndio wataniachia ili niende zangu Nigeria kwenye kikao cha wa wachungaji.”
Maneno hayo ya nabii Sanga yakamnyong’onyeza mrs Sanga. Hadi hapo akatambua kwamba mume wake ana tambua ni nini kinacho endelea na siri aliyo ihisi kwamba Tomas hato izungumza basi ipo wazi kwa mume wake.
“Ila sijui kwa nini aliye wapa kazi hakuhitaji kunia kwa kutumia watekaji wake. Ila nina hisi ana hitaji siku moja aje kuitoa roho yangu kwa mikono yake mwenyewe. Ila kabla ya yeye kufanya hivyo basi nita hakikisha kwamba nina itoa roho ya kibaraka wake aliye mpatia pesa za kwenda kuwalipa majambazi kisha nitaitoa roho yake. Au una semaje mke wangu hilo si wazo zuri eheee?”
Nabii Sanga alizungumza huku akimkazia macho mke wake. Taratibu mrs Sanga akakaa kitandani huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga kwani kila kitu kinacho zungumwa na mume wake kina muhusu yeye.
ITAENDELEA
Haya sasa, Nabii Sanga ameamua kutumia njia ya mafumbo kumfikishia ujumbe mke wake. Mrs Sanga sasa yupo kwenye wakati mgumu wa mawazo je ata kiri kwa mumewe kwa makosa aliyo yafanya? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 15.

0 Reviews