SIN 12

SIN 12

Author:
Price:

Read more

SIN 12
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
Website……………………………………………… www.storyzaeddytz.com
ILIPOISHIA
RPC akaifunua maiti moja na akamuonyesha Tomas maiti ya Selemani D iliyo chakaa kwa kupigwa risasi.
“Hawa jana tu walikuwa hai, wakisherekea pesa nyingi walizo zivuna kwa kumteka nabii Sanga. Ila sasa hivi wapo hapa hawajitambui. Wewe upo hai ila hii bastola yangu ina weza kukulaza na wewe hapa na ukajumuika na hawa wezako. Niambie ni wapi wezako walipo mpeleka nabii Sanga la sivyo, utaungana nao na wewe utaingizwa kwenye jokofu lile pale ukiwa maiti”
RPC alizungumza huku akimuwekea Tomas bastola ya kichwani na kumfanya Tomas kuanza kutetemeka mwili mzima huku akiona mwisho wa maisha yake sasa umefika, tena ana fia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.
ENDELEA
Kwa woga ulio mtawala Tomas akashindwa kuizuia haja ndogo na kujikuta akijikojolea. RPC hakulijali hizo zaidi ya kuendelea kuzungumza kwa ukali huku akiwa ameishikilia bastola hiyo.
“Kwa nini ulimteka nabii Sanga, nini alikufanyia ikiwa wewe ni mtu wake wa karibu?”
“Ehee…..!!”
“Nini alikufanyia?”
RPC alizungumza kwa ukali na kumfanya Tomas kuanza kukumbuka jinsi alivyo anza mahusiano na mke wa nabii Sanga. Kukolea kwa mapenzi yao kuliwafanya washiriki katika dhambi ya kumteka nabii Sanga ili wazuie mpango wake wa kumfungulia mgahawa na kumnunulia nyumba Magreth.
“Oya andaa hilo jokofu la hapo kwa ajili ya huyu mjinga, nina muua na siri itabaki kati yako mimi na wewe?”
RPC alizungumza huku akimtazama muhudumu wa Mochwari. RPC akaikoki bastola hiyo na kumfanya Tomas kuzidi kuweweseka. Japo ame fanya makosa, ila hatamani kabisa kufa.
“Nitasema ukweli”
Tomas alijikuta akiropoka na kumfanya RPC atoe simu yake mfukoni. Akaweka upande wa kurekodi sauti na kusubiria ukweli ambao Tomas ata ukiri.
“Zungumza nina subiria.”
“Ahaa miezi kadhaa iliyo pita nabii Sanga na mke wake walinipa jukumu la kuwatafutia eneo kubwa la kujenga mji, kule kigamboni. Jukumu la kusimamia mpango huo, alimkabidhi mke wake. Hivyo nilipata muda mwingi sana wa kuongozana na mke wake kwenda kutembelea maeneo mbali mbali ambayo nilikuwa nimeyapata.”
Tomas alizungumza huku akiendelea kutetemeka. RPC hakuishusha bastola yake, hii ni kuhakikisha kwamba Tomas ana zungumza kila kitu.
“Tulijikuta tukianza mahusiano ya kimapenzi na mwana mama huyo”
RPC akastuka sana ila hakuhitaji kuonyesha mstuko huo kwani ana hitaji kufahamu mambo mengi sana kutoka kwa Tomas.
“Tulifanya kwa siri sana. Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi penzi letu lilivyo zidi kuchanua. Kuna siku nabii Sanga alinipigia simu na kuniambia kwamba ana hitaji nimtafutie sehemu ya kufungua Mgahawa na nyumba ya kupanga maeneo ya Mikocheni. Alikuwa na mpango wa kumpangishia binti mmoja ambaye ni muumini pale kanisani kwake”
“Binti huyo ana itwa nani?”
“Magreth. Swala hilo nabii Sanga aliniomba nisimuambie mke wake kabisa. Ila kwa upande mmoja roho iliniuma kuona binti mdogo ana nunuliwa nyumba ya milioni mia tano. Nilimueleza mke wake na mkewe aka toa wazo la kumteka mume wake, hadi wiki ijayo ndio aachiliwe na watekaji ili aende nchini Nigeria kwenye kikao cha wachungaji na manabii”
RPC akajikuta akishusha pumzi taratibu. Katika miaka yote ya kuifahamu familia ya nabii Sanga, hakutarajia kwamba mke wa nabii huyo ipo siku ata fanya kosa kubwa kama hilo.
“Niliwatafuta vijana na nikawapa kazi hiyo na waliweza kuikamilisha kikamilifu”
Tomas alizungumza huku akiendelea kutetemeka kwa woga.
“Kwa hiyo mzizi wa tukio zima ni mke wa nabii SANGA?”
“Ndio”
Taratibu nabii RPC akashusha bastola yake na kuirudisha kiunoni mwake. Aka yahifadhi mazungumzo hayo ya Tomas kwenye simu yake na kuiweka mfukoni.
“Zirudishe hizo maiti”
Nabii Sanga alimueleza mtu huyo anaye hudumia Mochwari kisha wakatoka katika chumba hicho. Akamuingiza Tomas kwenye gari lake, kabla ya yeye kuingia, akatafuta namba ya kijana wake mmoja na kumpigia.
“Ndio mkuu”
“Upo wapi?”
“Bado nipo nyumbani kwa nabii Sanga.”
“Hakikisha huyo mke wake hatoki kwenda eneo lolote”
“Kwa nini mkuu?”
“Hupaswi kunihoji kwa nini, fwata amri yangu”
“Samahani sana mkuu.”
RPC akakata simu na kuingia ndani ya gari.
“Huyo Magreth ana ishi wapi?”
“Ahaa sifahamu, ila wale vijana mulio waua ndio walimfwatilia msichana huyo na kufahamu ni wapi ana fikishwa na nabii Sanga. Ila kwa mimi sijui”
RPC akamtazama Tomas machoni mwake kwa sekunde kadhaa na kuamini kwamba anacho kizungumza ni kitu cha ukweli. Nabii Sanga akawasha gari hilo na kurudi makao makuu ya polisi. Akakabidhi Tomas kwa vijana wake na akarudishwa mahabusu. RPC moja kwa moja akapitiliza hadi ofisini kwake, akajifungia na kuisikiliza sauti ya Tomas jinsi inavyo toa maelezo hayo.
“Haki ya Mungu hawa wanawake hawaaminiki”
RPC alifikiria huku akitafakari ni jinsi gani anavyo weza kuvumbua mbele ya jamii kesi hiyo ambayo kwa namna moja ama nyingine ina weza kwenda kuligawanya kanisa la nabii Sanga huku naye akiwa ni miongoni mwa waumini wa kanisa hilo.
***
Magreth akabaki kama alivyo zaliwa huku akimtazama nabii Sanga anaye malizia kuivua suruali yake. Akatembea taratibu hadi kitandani. Akamlaza nabii Sanga chali, kisha aka mkalia kiunoni mwake, huku taratibu akimzamisha jogoo wa nabii Sanga katika kitumbua chake. Aibu aliyo kuwa nayo awali, yote ime muondoka. Magreth kwa jinsi alivyo pagawishwa na kiasi cha pesa alicho pewa na nabii Sanga, hakuona haja kumbania mzee huyo, huku moyoni mwake akiamini kwamba swala zima la kumpenda Evans litakuja hapo baade akiwa amesha weka kila kitu sawa. Mtanange wa wakati huu hakuwa wa kinyonge, Magreth alijitahidi kardi ya uwezo wake kufanya vitu ambavyo hapo awali alikuwa akivisikia kwa marafiki zake wa mtaani wakivisimulia tu. Nabii Sanga alizidi kuchanganyikiwa na kupagawa na penzi bichi kabisa la Magreth.
“Nitakupa kila utakacho kitaka Mage”
Nabii Sanga alizungumza huku akiendelea kukatikiwa kiuno na Magreth ambaye ameamua kujitoa ili mradi mambo yake yamuende sawa.
“Kweli?”
“Haki ya Mungu vile, sijawahi kupata penzi tamu kama lako.”
“Uta nilinda dhidi ya mke wako?”
“Ndio baby, hawezi kukugusu”
“Niahidi”
“Nakuahidi, haki ya Mungu vile”
Magreth alifanya mahojiano hayo huku akikizungusha kiuno chake kama feni. Kuokoka kwake hakukumfanya ashindwe kumpagawisha nabii Sanga. Hadi mzunguko huo una kwisha kila mmoja akajikuta akiwa ameridhika na kiu ya mapenzi ikipungua kwa kiasi kikubwa.
“Wewe ni mtamu sana Mage”
“Asante mpenzi wangu”
“Niambie nini una hitaji nikufanyie?”
“Aahaa…kuna yule mgonjwa wangu kule hospitalini. Nilikuwa nina ombi moja”
“Ombi gani baby”
“Nimezungumza naye na amenieleza shida alizo pitia. Siku ile aliyo niokoa aliweza kuibiwa vyeti vyake vya kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu na siku ile aliondoka kwa rafiki yake na hakuwa na pakuishi. Nina omba nitakaopo hamia kwenye ile nyumba kigamboni, niweze kuishi naye”
Magreth alizungumza huku akiwa amejilaza kifuani mwa nabii Sanga na kuchezea chezea guarden love zake.
“Ahaha. Una muamini?”
“Kama aliweza kuyatoa maisha yake kwa ajili yangu. Nina muamini kwa maana wale Panya road siku zile wange nibaka na sijui ningekuwa kwenye maisha gani. Inawezekana ningekuwa nimesha kufa sasa”
“Nimekuelewa mke wangu. Basi akitoka hospitalini, utaishi naye. Ila hakikisha kwamba huni saliti”
“Kwa nini nikusaliti mpenzi wangu, ikiwa usichana wangu wewe ndio ume bahatika kuutoa. Au huniamini?
“Nakuamini tena sana kwa maana nime jionea jinsi gani ulivyo mtamu”
“Nashukuru mume wangu”
“Leo usiku nitarudi kwangu, ila hakikisha kesho una kwenda kununua asset zote za ndani kisha zinapelekwa kwenye hiyo nyumba mpya.”
“Sawa mpenzi”
“Kuna rafiki yangu mmoja ana kampuni ya magari. Nitamuambia kesho akutafutie gari zuri na lenye hadthi na wewe”
“Asante sana mpenzi wangu, ila mimi siwezi kuendesha gari?”
“Ohoo usijali katika siku hizi ambazo nita kuwa hapa Tanzania, nitakufundisha gari, hadi nina ondoka nina imani utakuwa umesha mudu kuendesha”
“Sawa sawa mume wangu”
Miili yao ilipo pata nguvu wakarudi tena kwenye mzunguko wa pili huku, kila mmoja akiwa amesha mzoea mwenzake.
***
‘Kama porini hakuweza kuonekana na majambazi tumewakuta wao wenyewe, je watakuwa wamemuaa? Hapana hajauwawa au wamemuachia?’
RPC aliwaza kichwani mwake huku akijaribu kujiongeza kutokana na mazungumzo ya Tomas.
‘Kama wamemuachia ata kuwa amekwenda wapi? Au ame fahamu kwamba mke wake ndio msaliti?’
‘Ila kama aliamua kumnunulia mwanamke nyumba ya milioni mia tano na kuhitaji kumfungulia mgahawa, nina imani kwamba atakuwa ana muamini sana huyo mwanamke na kumpenda’
‘Magreth…..Yaa Magreth anaweza kufahamu ni wapi alipo nabii Sanga. Ni lazima tumpate huyu msichna’
RPC baada ya kupata mwanga katika swala la kuto kumpata nabii Sanga, akanyanyuka kwa haraka na kuelekea mahabusu alipo fungiwa Tomas.
“Nileteeni mtu wa kuchora”
RPC alimuagiza bodyguard wake huku akimtazama Tomas ambaye amejikunyata kwenye kona ya chumba hicho.
“Nahitaji utuelezee sifa za Magreth. Si una mkumbuka kwa sura?”
“Ndio nina mkumbuka”
Polisi mwenye taaluma ya kuchora akafika eneo hilo. Tomas akaanza kuelezea muonekano wa Magreth.
“Ana sura nyembaba kiasi iliyo chongoka kwenye kidevu chake. Ana macho yaliyo kaa muundo kama wa yai, ila si makubwa. Ana pua ndogo ndogo kiasi na lipsi zake pia ni ndogo kiasi. Ni mrefu kama futi sita kasoro kidogo. Ana rangi ya chocolate fulani hivi.”
Kila alicho kieleza Tomas ndicho anacho kifanya mchoraji. Baada ya muda mfupi sura halisi ya Magreth ikapatikana kwenye karatasi ya mchoraji.
“Imekamilika?”
“Ndio mkuu”
RPC akaitazama picha hiyo ya Magreth, kweli ni mwanamke mzuri sana na anaye vutia. RPC akamgeuzia Tomas picha hiyo.
“Ndio huyu?”
“Ndio ndio huyo huyo wala hujakosea”
Tomas alizungumza wa kubabaika.
“Vijana wako hawakukuambia ni wapi walipeleleza hadi wakatambua anapo ishi?”
“Hapana hawakunijulisha kwani lengo lao kubwa ilikuwa ni nabii Sanga na waliweza kumfwatilia nabii Sanga alipo kuwa ana rudi kwake ndio waka mvamia na kumteka.”
RPC akaikunja vizuri karatasi hiyo yenye picha ya Magreth. Akaeleka kwenye kitengo cha askari wanao dili namitandano.
“Scan hii picha na unitafutie huyu binti”
“Sawa mkuu”
Kijana huyo aka iscan picha hiyo na kuiingiza kwenye computer yake na kuanza kutafuta picha hiyo ya Magreth kwenye mtandao. Haikuchukua muda maelezo yote kuhusiana na Magreth yakatokea katika computer hiyo. Imekuwa ni rahisi sana kwa askari hao kuipata kwani Magreth ni miongoni mwa Watanzania walio jisajili kwenye kitambulisho cha taifa hivyo taarifa zote zinazo muhusu yeye zipo hapo.
“Magreth Jonas Asenga”
RPC alisoma maelezo yanayo onekana kuhusiana na Magreth.
“Hembu tuma maelezo hayo kwenye mitando ya simu watupatie information za binti huyo. Nina imani mtandoa mmoja wapo utakuwa na information zake za mawasiliano.”
“Sawa mkuu”
Kijana huyo akaandika email kwa mitandoa mikubwa mmine ya mawasiliano hapa Tanzania, huku email hiyo ikwia huku ikiwa na wito wa kuomba data za mteja Magreth Jonas Asenga, ikiwemo namba yake ya simu. Baada ya dakika tano kijana hiyo akajibiwa email yake na mtandao wa simu ambao Magreth ana utumia.
“Waombe simu zote zilizo pigwa jana na leo watutumie”
Maombi hayo hayakuweza kukataliwa kwa maana yana tokea makao makuu ya polisi. Wakaanza kuorozesha audio za mazungumzo yote aliyo yafanya Magreth kwa siku ya jana na leo. Wakaanza kusikiliza mazungumzo hayo ambayo yanamuhusisha Magreth na nabii Sanga ambaye alimpa maelekezo ya kwenda kuchukua pesa ofisini kwake. Wakazidi kuendelea kusikiliza mazungumzo hayo hadi jinsi MagreLth aivyo wasiliana na majambazi hao na kuwajulisha amefika Mkinga.
Mazungumzo ya siku ya leo kati ya nabii Sanga na muhasibu wake akimuomba amfwate sehemu alipo, ikampa picha RPC ya kuweza kufahamu kwamba nabii Sanga yupo sehemu gani na yupo sehemu salama. Ila kutokana ni ahadi ambayo alitoa kwa wananchi kwamba jeshi la polisi lita hakikisha kwamba lina mrudisha nabii Sanga salama salmini mikononi mwa familia yake. Ikamlazimu RPC kuandaa kikosi cha vijana wake wanne na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwa Magreth, huku zoezi hilo likifanyika kwa siri sana pasipo askari wengine kuweza kufahamu ni kipi RPC wao ame kigundua.
ITAENDELEA
Haya sasa, RPC ana elekea nyumbani kwa Magreth je watafanikiwa kumkumta nabii Sanga? RPC je atafungua kinywa kutoa siri juu ya mtekaji halisi wa nabii Sanga ni Mrs Sanga? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 13.

0 Reviews